Command Centre / Press Room / Tourism
TourismTuesday, 1 September 2026 · 2 min read
NKURINGO GORILLA LODGE YA UGANDA YATUZWA NA WTA ZANZIBAR

Na Monday Akol Amazima
Nkuringo Gorilla Lodge ni mojawapo wa kampuni na mashirika yaliyopewa tuzo zisiwani Zanzibar tarehe 28 Agosti 2026 katika hotel mpya ya kifahari ya Diamonds Bijoux Zanzibar Resort iliyopo Bwejuu. Katika sherehe hiyo ya kuwatuza waliobora zaidi barani Afrika, asasi ya World Travel Awards (WTA) ilitoa tuzo mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoteli, usafiri wa anga na utalii.
Katika sekta ya hoteli Nkuringi Gorilla Lodge ilipewa tuzo ya kutoa huduma bora za malazi kwa watalii wanaokuja Uganda hasa wale wanaoenda kuona sokwe (Gorilla) katika mbuga za Wanyamapori za Bwindi na Mgahinga.
Katika sekta ya usafiri wa anga, mashirika ya ndege ya Ethiopian Airlines, Rwanda Air na Kenya Airways yalituzwa kuwa mashirika bora zaidi ya usafiri wa anga barani Afrika. Mashirika haya yalisifiwa kwa kuwa na huduma bora kwa wateja na kufuata bila kuchelewa ratiba yao kama inavyotolewa kwa wasafiri.
Katika upande wa kumbi bora za makongamano, Durban ICC ya Afrika Kusini ilituzwa kama kituo cha ukumbi wa makongamano bora pa kufanyia mikutano ya kimataifa. Kwa upande wa mbuza za Wanyama, Serengeti na Kilimanjaro zilichaguliwa kuwa bora zaidi barani Afrika kwa vile huwavutia watalii wengi.
Zanzibar wenyeji wa sherehe hii waliweza kupata tuzo ya kuwa eneo lenye bichi bora zenye kuvutia 2026 na vilevile eneo lenye kufanya matamasha yakuvutia 2026
Asasi ya World Travel Awards ilianzishwa 1993 na Graham E. Cooke ikiwa na lengo la kutambua, kutoa zawadi na hamasa kwa wale wanaotoa huduma bora zaidi katika sekta za usafiri, hoteli na utalii. Tuzo hizi huchangia pakubwa wakati wasafiri wanapokuwa wanachagua aina ya usafiri na mahali pa kuishi.
Kwa upande wmingine baraza la mawaziri Uganda katika kikao kilichifanyika ikulu tarehe 31 agosti 2026 waliridhia Uganda kuadhimisha siku ya utalii duniani itakayofanyika tarehe 27 Septemba 2026.
Kulingana na Waziri wa TEHAMA na Uelekezaji wa Taifa Mhe. Justine Kasule Lumumba maadhimisho yatafanyika jijini Mbale mashariki mwa Uganda na mgeni rasmi atakuwa Rais Yoweri Museveni. Kuadhimisha siku hii ni mojwawapo wa juhudi za kukuza sekta ya utalii Uganda huku watalii wakihamasishwa kuzuru Ugandan kwa vile kuna vivutio vingi vya utalii. Mwandishi ni Mkuu wa Dawati la Kiswahili Kituo cha Habari Uganda
: - Graham Cooke wa WTA akitoa tuzo kwa wajumbe kutoka Nkuringo Gorilla waliotuzwa kama Safari Lodge iliyobora zaidi nchini Uganda 2026


